[Wako mwana ukamtuma, duniani
Kisa na maana nipate uzima jamani] x2
[Ishara ya kwamba unanipenda zaidi
Hivyo nishaelewa sifa nitakupa zaidi] x2
Chorus:
[Na siwezi jizuia, kusema wako wema
Na sio kama najigamba, umenitenda mema]x2
Umekuwa mwema kwangu
Umenitoa gizani, nilipokuwa nimeshikwa mateka
Ukanipa tumaini, kwako nikajificha
Sasa nitakupa nini, iwe sawa na yale umenitenda?
Hakuna ila moyoni, sifa nitakuimbia
Ilikugharimu, msalabani unifie
Hivyo inanibidi, sifa nikuimbie
Wema wako niseme, ili na wengine wakujue
Wote waungane nami, na wazee ishirini na nne
Chorus
0 comments
Post a Comment