Tabibu Lyrics – Angela Chibalonza


Ni tabibu wa karibu, tabibu wa ajabu
Na neema na daima, ni dawa yake njema
Hatufai kuwa hai wala hatutumai
Ila yeye kweli ndiye atupumzishaye

Imbeni malaika sifa za Yesu Bwana
Pweke limetukuka jina lake Yesu
X2

Dhambi pia na hatia ametuchukulia
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni
Uliona tamu jina la Yesu Kristu Bwana
Yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa

Kila mume asimame sifa zake zivume
Wanawake na washike kusifu jina lake

0 comments

Post a Comment