Bwana Ni Mchungaji Wangu Lyrics - Reuben Kagame


Bwana ni mchungaji wangu,
Sitapungukiwa kitu
Hun’laza penye majani mabichi,
Huniongoza kwa maji matulivu

Chorus
Hakika wema nazo fadhili zitanifuata mimi,
Nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu

Hunihuisha nafsi yangu,
Hun’ongoza kwa njia za haki
Nipitapo bondeni mwa mauti,
Sitaogopa wewe u nami

Gongo lako na fimbo yako,
Vitanifariji mimi
Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu

6 comments: